Connect with us

Download Audio: Luckson Daniel – Fanya

Muziki

Download Audio: Luckson Daniel – Fanya

Shalom mwana wa Mungu! leo kupitia mtandao wako pendwa wa gospomedia leo nimekuletea wimbo uitwao FANYA kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili za kisasa (Contemporary Gospel) anayefahamika kwa jina la Luckson Daniel kutoka jijini Dar es salaam, wimbo huu umetengenezwa ndani ya studio za HM Records chini ya mikono ya prodyuza Maka-Rhythm.

Fanya ni wimbo wa unyenyekevu na wenye kutia nguvu ya Imani mbele za Mungu ukitukumbusha jambo muhimu kwa sisi wana Mungu ambao mara nyingi tumekuwa tukilalamika na kunug’unika juu ya matatizo na majaribu tunayopitia ambayo kwa namna tofauti tofauti yamekuwa yakitusogeza mbali na Mungu na leo kupitia wimbo huu wa ”FANYA” mwimbaji Luckson Daniel anatukumbusha kuwa ni muda sasa umefika wa kurudi kwa Bwana Yesu Kristo ili aweze kutuhuisha na kubeba mizigo ya matatizo yetu na jambo hili litafanyika pale tu ambapo utaamua kurudi kwa Mungu na kumruhusu afanye kile ambacho kitakutoa pale mahali penye ugumu na kukupeleka mahali patakatifu ukiwa na ujazo wa baraka zisizo na kikomo katika maisha yako.

Baadhi ya mashairi yanayopatikana kwenye wimbo huu:

Verse
Bora wakukatae,,bora wakutenge ili uinuliwe na Mungu mwenyewe.
Uliyekua naye jana,, haupo tena naye Leo..
Chozi lako linapodondoka (usisahau kumkumbusha Mungu)..
Jambo gani unalolitaka ( Maana kwa Mungu hakuna gumu)
Mwambie babaaaaa!..

Chorus
Fanya Fanya Fanya
Hakuna linalokushinda were
Fanya Fanya I need you papa God ooh..×3

Hii ni moja kati ya nyimbo zenye kubariki sana unaposikiliza, Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza wimbo huu ambao ni hakika utakwenda Kufanya jambo kuu katika maisha yako leo.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Luckson Daniel kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 714 255 432
Facebook: Luckson Danie | Youtube: Luckson Daniel
Instagram: @lucksondaniel_gospelhuru

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top