Connect with us

Download Audio: Joel Lwaga – Pendo

Muziki

Download Audio: Joel Lwaga – Pendo

Kutoka jijini Dar es salaam, leo kupitia blog yako pendwa ya gospomedia tumekusogezea wimbo mpya uitwao Pendo kutoka kwa mwimbaji mahiri na anayefanya vizuri sana katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Joel Lwaga wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Push Up Records.

Pendo ni wimbo wa kiwango cha juu kabisa katika kutia moyo na kuongeza tumaini ndani ya nafsi na roho ukielezea Upendo wa Mungu kwa wanadamu, kupitia wimbo huu mtumishi wa Mungu Joel Lwaga anatufundisha na kutukumbusha ni kwa jinsi gani upendo wa Mungu unavyotufanya tuwe na uhai halisi uliojaa ukamilifu wa furaha isiyo na kikomo,  nguvu isiyo na kipimo na hapa ndipo palipo na Pendo halisi la Mungu linalojidhihirisha na kutufanya kuwa wenye kuishi kwa kusudi lake… huu ni wimbo uliojaa baraka sana kwa wote wanaoamini katika wokovu wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kwa upendo wa Mungu alipewa uwezo wa kukubali kuteswa na kufa msalabani kwa ajili ya kusafisha dhambi zetu na hayo yote yalikamilishwa na Pendo la Mungu Baba.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu wenye mafuta ya pekee ya baraka yatakayobadilisha maisha yako na maana halisi ya Pendo itakuwa imejidhihirisha juu yako. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Joel Lwaga kupitia
Simu/WhatsApp: +255 716 747 597
Facebook: Joel Lwaga
Instagram: @Joellwaga_official
YouTube: JoelLwaga

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

 

GUARDIAN ANGEL - NI TABIBU_audio

Muziki

AUDIO | GUARDIAN ANGEL – NI TABIBU

By September 22, 2021

TRENDING

To Top