Connect with us

Download Audio: Chris Shalom – Dry Bones Are Rising

Muziki

Download Audio: Chris Shalom – Dry Bones Are Rising

Shalom mwana wa Mungu! leo kutoka nchini Nigeria tumekusogezea wimbo mpya uitwao ”Dry Bones Are Rising” kutoka kwa muimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchini humo na afrika kwa ujumla anayefahamika kwa jina la Chris Shalom.

Licha ya Chris Shalom kuwa muimbaji binafsi pia ni kiongozi wa nyimbo za kuabudu ambaye mara nyingi amekuwa baraka kwa watu wengi ambao wanafuatilia nyimbo zake hasa awapo madhabahuni akihudumu kwa kuwa inaaminika kuwa nyimbo anazoimba zinakuwa zimebeba nguvu kubwa ya kiroho na kuinua nafsi za watu wengi zaidi ndani na nje ya Afrika.

Wimbo huu umetayarishwa kwenye mahadhi ya kisasa ya muziki wa Injili na huu ni mfululizo wa nyimbo anazoendelea kuziachia kutukoa kwenye mkusanyiko maalumu wa nyimbo hizo alioupatia jina la ‘Worship in Every Place Series’

Chris alisisitiza kwamba atakuwa anaendelea kuachia nyimbo zaidi kutoka kwenye mfululizo wa nyimbo hizo na wimbo huu umekuja baada ya kuachia wimbo uitwao ”My Beautifier” miezi michache iliyopita.

gospomedia.com tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu wa kuabudu ambao tunahakika utakubariki sana. Karibu!!

Download Audio

Social Media:
Facebook: Chris Shalom
Instagram: @chrisshalom_thegoldenvoice
Twitter: @shalom_chris
Web: chrisshalomonline.com

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Continue Reading
Advertisement
You may also like...
Advertisement

TRENDING

To Top