Audio

Audio: Dona Jr. feat. Rebecca – Narudi

Baada ya kuachia albamu yake mpya iitwayo Sihitaji Refa, rapa wa nyimbo za Injili kwa mtindo wa HipHop akifahamika kwa jina la Dona akitokea jijini Dar es salaam, leo ametambulisha wimbo wake mpya uitwao Narudi akiwa amemshirikisha mwanadada Rebecca, wimbo huu umetayarishwa ndani ya studio za Enzi Records chini ya mikono ya prodyuza Amzy.

”Narudi ni wimbo unaolezea mtu aliyepotea na inafika wakati anaamua kurudi kwa Yesu Kristo baada ya kuhangaika sana kama ilivyo katika hadithi ya mwana mpotevu. Na jumatano ni jumatano kuu ya majivu ambapo tunaanza kipindi cha kwaresma kuelekea Pasaka kikiwa ni kipindi ambacho dhima yake kubwa ni kurudi kwa Mungu kama asemavyo Yoel 2:12 – ”lakini hata sasa asema Bwana Nirudieni Mimi kwa mioyo yenu yote.” – Alisema Dona.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu na hakika utakwenda kukubadilisha na kukubariki. Karibu!!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko wasiliana na rapa Dona JR kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 746 083 735, +255 713 02 44 55
Facebook: Donanciano Van Joseph
Instagram: @255dona
Twitter: @255dona
Youtube: DONA Jesus Rapper

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Ben Jonathan - Siteketei & Salama (Mashup)

Next post

Video | Audio: Yohana Mpangule - Nibariki