Audio: Dona JR - Nashusha Nyavu - Gospo Media
Connect with us

Audio: Dona JR – Nashusha Nyavu

Audio

Audio: Dona JR – Nashusha Nyavu

Baada ya wiki chache zilizopita kuachia video ya wimbo wake uitwao Tumsifu Yesu Kristo kwa mara nyingine tena rapa wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania maarufu kama Dona JR ameachia wimbo wake mpya uitwao Nashusha Nyavu.

Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Enzi Records chini ya mikono ya prodyuza Crisbeats.

“Nashusha nyavu ni wimbo unaoelezea kazi aliyotutuma Bwana Yesu alipowaambia mitume wake Marko 16:15 Akawaambia , Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri injili kwa kila kiumbe.

Na luka 5:4 hata alipokwisha kunena alimwambia Simoni , tweka mpaka kilindini mkashushe nyavu zenu mvue samaki.

Luka 5:10
Na kadhalika Yakobo na Yohana wana wa Zebedayo , walikuwa washirika wa Simoni. Yesu akamwambia Simoni, Usiogope , tangu sasa utakuwa ukivua watu.

Kwahiyo nashusha nyavu ni wimbo ambao unatukumbusha wajibu wetu kama wakristo wa kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi wa Yesu.” – alisema Dona

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu tukiamini kuwa utakubariki na kugusa kwa namna ya kipekee, Ameen.

Kwa watumiaji wa tovuti bonyeza hapa chini:

Download Audio

Kwa watumiaji wa App bonyeza hapa chini:
Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na rapa Dona JR kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 746 083 735, +255 713 02 44 55
Facebook: Donanciano Van Joseph
Instagram: @255dona
Twitter: @255dona
Youtube: DONA Jesus Rapper

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top