Habari

Director Einxer,Pyuza,Kilonzo kukutana ndani ya Tamasha la The Big Praise Concert Dar June 18

Waandaji wa Tamasha la The Big Praise Concert Balozi wa Vijana Tanzania na YTDO wamesema kuwa Tamasha la The Big Praise Concert ambalo litakutanisha kada zote za muziki huo wakiwemo waimbaji, watangazaji, producer na director mbalimbali ambao ni familia ya muziki wa injili hapa Tanzania bila kuwasahau mashabiki wa muziki huo hapa nyumbani.

Akizungumza na Gospo Media Mkurungezi wa taasisi ya Balozi wa vijana Tanzania ndugu, Johnson Jackson amesema kuwa lengo ni kuwaleta wana wa Mungu pamoja kusifu kwa pamoja na kufahamiana zaidi na wale ambao huwa wanawafanyia kazi zao na wale ambao huwa wanasikiliza kazi hizo na maandalizi ya Tamasha hilo yameshakamilika na madirector kama Pyuza na Einxer wameshathibitisha uwepo wao na sasa kinachosubiriwa ni siku yenyewe ifike watu waje kumsifu Mungu na watu wanaowapenda.

Mpaka sasa ninapozungumza na wewe kila kitu kipo tayari kama ni mwari basi anasubiriwa kutoka ili watu waweze kula wali wa shughuli yenyewe,taarifa kwa waimbaji ambao watashiriki Tamasha hili tayari wote wamekubali na watakuwepo siku ya tukio na mbali na waimbaji watangazaji ambao tayari wameshakubali kushiriki ni pamoja na Bony Magupa wa Praise Power Radio,Hossein Gabrieli wa Praise power Radio,David Gille wa WAPO RADIO,Ritha Chuwalo wa EA Radio na wengine wengi,mbali na watangazaji hao waimbaji wakongwe kama Rebecca Magaba,Tumaini Njole nao watakuwepo na waimbaji wengim wote ambao wapo kwenye tangazo wamekubali kushiriki kwao pia mbali na hao directors kama einxe na pyuza watakuwepo pia Maprodecer wakongwe na maarufu Eck  na PG ambao wamefannya kazi za akina Rose Muhando na Bahati Bukuku,hivyo hili ni zaidi ya tamasha mtu asibaki kwao“.Alisema Johnson

Tamasha hilo litasheni vitu mbalimbali kama Comedi kutoka kwa Ekwis Kicheko ambaye anafanya vyema kwa upande huo wa uchekeshaji,Tamasha la The Big Praise Concert linatarajiwa kufanyika siku ya tarehe 18-06-2017 pale katika kanisa la Fpct-kurasini Mkabala(jirani)na viwanja vya Sabasaba Maonyesho kuanzia saa saba mchana na kuendelea hakuna kiingilio.

Mawasiliano na Balozi wa Vijana Tanzania;

 

Simu/WhatsApp: +255 653 231 198, +255 655 33 49 49
Instagram: @johnsonjackson63
Facebook: Johnson Jackson Facebook Page: Balozi wa Vijana Tz.
Youtube: Johnson Jackson

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

 

Advertisements
Previous post

Mwimbaji Beatrice Muhone awashangaa wasiotaja Jina la Yesu Hadharani

Next post

Joe Praize awaalika Mashabiki kwenye Harusi yake june 17 mwaka huu.