Audio

Audio: Deusdedith Peter Feat. Neema Ng’asha – Asante

Kutoka jijini Mwanza leo kwa mara nyingine tena nimekuletea wimbo mzuri sana uitwao Asante kutoka kwa muimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Deusdedith Peter safari hii akiwa amemshirikisha mwimbaji anayefanya vizuri jijini Mwanza anayefahamika kwa jina la Neema Ng’asha. Wimbo huu umefayika ndani ya studio za Over The Classic chini ya mikono ya prodyuza David Cosmas.

Huu ni wimbo wa shukrani unaotukumbusha jambo la kumshukuru Mungu katika maisha yetu kwakuwa Mungu amekuwa mwema katika kila jambo letu, katika kila hatua na katika yote kupitia Yesu Kristo ambaye amekuwa akitenda mambo mema kila siku katika maisha yetu kupitia msaada wa Roho Mtakatifu ambaye yupo nasi hata sasa. Naamini kupitia wimbo huu utakuwa umejifunza jambo la kumshukuru Mungu na kumtukuza kila siku kwakuwa amekuwa mwema kwako kila siku.

Akizungumza na gospomedia.com kwa upande wake mwimbaji Neema Ng’asha amesema kuwa

”Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kushirikishwa katika wimbo huu ambao nina hakika utakwenda kuwabariki watu wengi, Binafsi nilikubali kushiriki katika wimbo huu kwasababu napenda kuwatia moyo vijana na kuwainua hasa kwenye uimbaji wa muziki wa Injili kwa maana hata mimi nilianza kuimba tangu nikiwa kidato cha pili hivyo naelewa changamoto ambazo waimbaji wapya wanakutana nazo kila wanapotaka kupiga hatua ndio maana kwangu imekuwa rahisi kusikia kilio chao na kuwasaidia pale ninapoona naweza kufanya hivyo na napenda kusisitiza kwamba kwa yeyote mwenye kipaji cha uimbaji wa muziki wa Injili asisite kunitafuta kama yuko Mwanza tutafanya kazi wote na kama yuko mkoani naomba tuwasiliane kwa namba zangu za simu +255 673 527 249 nitamshauri, Maono yangu ni kuinua vipaji vya vijana kama hawa kwenye huduma ya uimbaji.” – Alisema Neema Ng’asha
Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu na hakika utabarikiwa. Ameen!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Deusdedith Peter kupitia
Simu/WhatsApp: +255 757 947 616
Facebook: Deuces Peter
Instagram: @deucespeter

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Inno Shaudo - Mungu wa Ajabu

Next post

Video: PeaceKing David Feat. Neema Gospel choir - Jesus you are my King