Connect with us

Video: Cornelio Stephano – Jishushe

Cornelio Stephano - Jishushe

Muziki

Video: Cornelio Stephano – Jishushe

Cornelio Stephano - Jishushe

Kutoka jijini Mbeya Tanzania kwa mara ya kwanza katika mwaka 2019 tunamtambulisha kwako mwimbaji Cornelio Stephano na hii ni video yake mpya na ya kwanza kabisa kuachia inayokwenda kwa jina la Jishushe.

Video hii imeongozwa director Azalia, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Fighter Records chini ya mikono ya prodyuza Fighter.

“Wimbo huu wa JISHUSHE ni wimbo mzuri ambao unatufundisha nguvu ya toba ya kweli mbele za Mungu na pia inafafanua jinsi gani maombi ya toba ya kweli ya mtu muovu yanavyomshawishi Mungu na kusimamisha maserafi na makerubi wasimsifu kwanza kwasababu mmoja aliyeamua kufanya toba ya kweli, Katika wimbo huu pia nimetoa mfano halisi wa watu waliojikinai na kujihesabia haki mbele za Mungu na kusahau kwamba watu wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” – alisema Cornelio

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema tukiamini kuwa itakubariki na kukugusa kwa namna ya pekee, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na Cornelio Stephano kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 753 857 736
Facebook: Cornelio stephano
Instagram: @minister_corneliostephano
Youtube: Cornelio Stephano

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

To Top