Mafundisho

COMMITMENT(AHADI) SOMO KUTOKA KWA MCHUNGAJI ELLY DAVID.

Shalom leo kupitia tovuti ya gospomedia.com tumekuletea video ya somo kutoka Mchungaji Elly David kutoka Tanzania somo hili linahusu AHADI(commitment) kupitia somo hili Mchungaji Elly David amezungumzia juu ya kuishi kwa ahadi ambazo tunajiwekea juu ya vitu au mambo tunayotaka tuyafikie au kufanikiwa na hapa mchungaji Elly David amesisitiza zaidi juu kutokata tamaa kutokana na changamoto tunazokutana nazo katika maisha yetu ya kila siku na kuhimiza zaidi kuishi kwa imani na kumtegemea Mungu ili kufikia maono ya ahadi uliyojiwekea katika kufika pale unapataka ufike na hakika kupitia video hii kutoka kwa Mchungaji Elly David utaweza kubarikiwa sana na  kukusaidia kukupa mwanga wa Matumaini mapya katika maisha yako.

Elly David ni kijana na ni Mchungaji wa kimataifa, ambaye alianza kuhubiri injili katika umri mdogo sana na kadri alivyokuwa anaendelea kukua alianza huduma ya kuhubiri Injili katika mitaa mbalimbali kwa kufanya mikutano na semina na mpaka kufikia sasa ameweza kuanzisha na kuendesha vipindi vya Radio na TV sehemu mbalimbali duniani ambapo kupitia mahubiri yake Mungu amempa kibali cha kubadilisha Maisha ya watu sio tu Afrika lakini pia katika nchi nyingi duniani.

Kutana na Pastor Elly David mhamasishaji wa vijana na maisha mchungaji huyu yupo tayari kukusaidia wewe kijana uliyekata tamaa na maisha katika nyanja zote za maisha kama , elimu, uchumi ,mahusiano na mengine mengi. Vile vile hutumika kwenye makongamano na semina mbalimbali kuwawezesha vijana kubadili mitazamo hasi ya kimaisha waliyonayo na kuwa chanya.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuzungumza na Mchungaji Elly David kupitia namba +255688440029, Email:keepthedream.david@gmail.com, au pia unaweza kuwasiliana naye kupitia mitandao ya kijamii Facebook: Elly David, Instagram: @ellydavid1 YouTube: Elly David na Office ya Mchungaji Elly David inapatikana Mbezi beach Tank bovu.
Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

DOWNLOAD AUDIO: WABA SHADRA FEAT JOYCE ALINE-TUMSIFU BWANA RMX

Next post

DOWNLOAD MUSIC AUDIO: STEPHEN WANDERA-WANADAMU JAMANI