Video

Video | Audio: Christina Shusho & Saint Stevoh – Mifupa Mikavu

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu, leo naitambulisha kwako video mpya iitwayo Mifupa Mikavu kutoka kwa mwimbaji mkongwe Christina Shusho akiwa na rapa wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya anayefahamika kwa jina la Saint Stevoh video hii imeongozwa na director Nezzoh Monts, na muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Teddy B kutoka jijini Nairobi.

Mifupa Mikavu ni wimbo uliotoka katika andiko la kitabu cha Ezekiel 37

1; Mimi Ezekieli nilikumbwa na uzito wa nguvu ya Mwenyezi-Mungu, naye akaninyanyua kwa roho yake na kuniweka katika bonde lililokuwa limejaa mifupa. 2; Basi, akanitembeza kila mahali bondeni humo. Kulikuwa na mifupa mingi sana katika bonde lile, nayo ilikuwa mikavu kabisa. 3; Mwenyezi-Mungu akaniuliza, “Wewe mtu! Je, mifupa hii yaweza kuishi tena?” Nami nikamjibu, “Ee Bwana Mwenyezi-Mungu, wewe wajua!” 4; Naye akaniambia, “Toa unabii juu ya mifupa hii. Iambie hivi: Enyi mifupa mikavu, sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu. 5; Bwana Mwenyezi-Mungu awaambia hivi: Nitaifanya pumzi iwaingie, nanyi mtaishi. 6; Nitawatia mishipa na nyama, nitawafunika ngozi na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. Hapo mtajua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao nina imani kubwa kuwa utakubariki.!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Christina Shusho kupitia
Facebook: Christina Shusho
Instagram: @christinashusho

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Waba Shadra - Jina Lako

Next post

Audio: Silvabel - Washa