Habari

Christina Shusho Kuja na filamu mpya hivi Karibuni

Mwimbaji mkongwe wa muziki wa injili Tanzania Christina Shusho anataraji kutoa Filamu mpya hivi karibuni na kuwashirikisha watu mbalimbali katika fialmu yake hiyo.

Akizungumza  mara baada ya kumaliza uzinduzi wake alipokuwa akifanyiwa mahojiano na moja ya waandishi wa Gospo Tv alisema kuwa sasa yupo mbioni kufanya filamu ambayo itawainua watu kiroho na kimwili na kuwajenga katika maadili mema.

Unajua kwasasa soko la Bongo Movie linakufa hivyo tunasubiriwa sisi watumishi kufanya kwa sehemu yetu,na nimejipanga kweli kweli kuja na filamu za kiinjili ili ziweze kutazamwa na familia za kipendwa ambapo rika zote wataangalia bila tatizo lolote,mfano mzuri ni ule wimbo wangu wa Waranda mbao ni story ndefu lakini unaona imekaa ndani ya dakika nne,so nipo njiani kuachia hiyo filamu miezi ya hivi karibu“Alisema Shusho

Na katika soko la Muvi za Injili za Tanzania Christina Shusho si wa Kwanza kwani alianza Jeniffer Mgendi na baadae Bahati Bukuku na sasa Christina Shusho.

Kwa mawasiliano na Christina Shusho

Facebook;Christina Shusho

Page Facebook;Christina Shusho

Instagram;Christina Shusho.

Instagram;Ze muhubiri

Advertisements
Previous post

Tazama Video | Download Music Audio: Mireille Basirwa - We Ndio Mungu

Next post

Habari: Mwimbaji Vaileth Mwinuka Aachia Album Yake Rasmi.