Christina Shusho Ataka Idadi ya Waimbaji Vijana Iongezeke. - Gospo Media
Connect with us

Christina Shusho Ataka Idadi ya Waimbaji Vijana Iongezeke.

Habari

Christina Shusho Ataka Idadi ya Waimbaji Vijana Iongezeke.

Mwimbaji mkongwe wa muziki wa Injli Afrika Mashariki na kati Christina Shusho anatamani kuona idadi ya waimbaji vijana ikiongezeka ili waweze kumtumikia Mungu wakiwa bado wakiwa na nguvu zao kabla hawajazeeka au kuchoka.

Akizungumza na GOSPOMEDIA.COM, alisema kuwa idadi ya vijana ikiongezeka ufalme wa Mungu utazidi kuwa na nguvu kila siku kwasababu vijana ndio wanazo nguvu za kumshinda mwovu shetani. Akimtolea mfano mzuri mwimbaji anayekuja kwa kasi ya aina yake Ikupa Mwambenja alisema kuwa Ikupa ni mwimbaji kijana ambaye amechagua fungu lilio jema la kumtumikia Mungu akiwa bado angali kijana mdogo.ihgf

‘Na sisi kama Mama au dada yake tupo tayari kushirikiana naye kwa hatua moja hadi kufikia malengo yake kuhakikisha tunamsapoti hivyo niwaombe sana waimbaji wa muziki huu wa injili hasa vijana wanaotaka kumtumikia Mungu wajitokeze mapema ili wasije wakaja kumtumikia Mungu wakiwa washachoka au kuzeeka ambapo nguvu zao zitakuwa zimekwisha hivyo wajitokeze mapema ili wafanye kazi ya Mungu pamoja nasi natamani sana kuona idadi ya vijana ikiongezeka“Alisema Christina Shusho.

Christina Shusho aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa albamu ya Ikupa Mwambenja  Jijini  Mbeya inayoitwa ADONAI yenye jumla ya nyimbo nane katika ukumbi  wa Mkapa Hall na kuhudhuliwa na Maelfu na waimbaji mbalimbali kama vile Upendo Nkone, Moses Simkoko, Tumaini Mbembela, Festina Mwandwanga, Happy Kamili na Upendo Sapali na waimbaji wengi.

Hivi ndivyo mwimbaji Christina Shusho alivyohudumu siku hiyo:

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

More in Habari

To Top