Connect with us

Audio: Chris Msaki – Songa Mbele

Muziki

Audio: Chris Msaki – Songa Mbele

Kutoka jijini Dar es salaamm leo kwa mara nyingine tena nimekuletea wimbo uliobeba ujumbe wa kukuinua uitwao Songa Mbele kutoka kwa muimbaji anayefahamika kwa jina la Chris Msaki, Wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za JB Production chini ya mikono ya prodyuza Baraka.

Kuna nyakati ambazo mtoto wa Mungu unakumbwa na majaribu mengi kiasi ambacho unahisi moyo kushuka na kuona safari yako ya maisha imeishia hapo lakini leo kupitia wimbo huu napenda kukumbusha jambo moja kubwa na la msingi kulishikilia katika maisha yako jambo hilo ni kumpata Yesu Kristo ambaye mbali na kushusha mizigo yako na kukupumzisha pia atakupa furaha na amani ya milele itakayokufanya kumtukuza Mungu kwa namna ya tofauti kabisa.

Nakusihi fanya uamuzi huu leo wa kumkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yako na Mungu atakwenda kutenda miujiza katika maisha yako leo hii!

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao nina imani utaufurahia na kukuinua. Barikiwa!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Chris Msaki kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 717 603 618
Facebook: Chris Philipo Msaki
Instagram: @chris_philipo_msaki
Twitter: @chris_philipo_msaki
Youtube: Chris Philipo Msaki

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top