Audio: Chichi Frank - Mimi Kwako - Gospo Media
Connect with us

Audio: Chichi Frank – Mimi Kwako

Audio

Audio: Chichi Frank – Mimi Kwako

Kutoka jijini Dar es salaam leo tumekusogezea wimbo mzuri unaokwenda kwa jina la Mimi Kwako kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Chichi Frank.

Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Sweseka Production chini ya mikono ya prodyuza Sweseka.

Mimi Kwako ni wimbo wa kukiri kuwa Yesu ni Bwana baada mtu kupita mahali fulani pasipo faa na kutambua kuwa Yesu ndiye Bwana na mwokozi wa maisha yake, haijalishi ni mangapi tunapitia, mara ngapi tunatenda dhambi lakini tunachopaswa kutambua ni kwamba kwa Mungu sisi bado ni watoto wake pale tunapohitaji kurudi kwake yeye hutupokea kutusamehe na kutufanya upya kwa ujazo wa Roho mtakatifu.

Ni hakika wimbo huu utakubariki kila wakati utakapokuwa unasikiliza na kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Chichi Frank kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 753 873 003
Facebook: Chichi Frank
Instagram: @chii_frank
Youtube: CHICHI FRANK TV GMF

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top