gospomedia.com ni blogu ya kikristo inayotoa huduma ya habari za kikristo na kurusha matangazo ya nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Lengo kuu la kuanzishwa kwa blogu hii ni kusaidia jamii kupata habari mbalimbali za kikristo zinazojiri duniani kote kila leo, nyimbo na video za muziki wa Injili ikiwa ni mkakati maalumu wa kuihamasisha jamii kuwa karibu na Mungu, kudumisha amani na upendo baina ya jamii bila kujali dini, kabila, ujinsia au utaifa wao.

Kupitia mafundisho ya kiroho, mahubiri na makala za maarifa ya kijamii kama vile afya, vijana, uchumi, mahusiano, sheria n.k jamii itapata kufunguliwa kiroho na kimwili kwa kupata ufahamu mpya.

Mbali na huduma ya habari, makala na matangazo ya nyimbo na video za muziki wa Injili, Blogu hii pia inazisaidia taasisi mbalimbali za kiroho kama vile makanisa, mashirika na watu binafsi kutangaza huduma zao na kuwasilisha ujumbe wao kwa jamii inayokusudiwa.

Blogu hii inamilikiwa na kampuni ya Gospo Media ambayo imesajiliwa na kutambulika kisheria nchini Tanzania, yenye makao yake makuu Magomeni, jijini Dar es salaam.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazotolewa na Gospo Media wasiliana nasi kupitia:

Simu: +255 658 293 696, +255 679 433 323
WhatsApp: +255 755 038 159
Facebook: Gospo Media
Instagram: @gospomedia
Twitter: @gospomedia
Email: gospomedia@gmail.com

Advertisements