Audio: Bliss Asikoko - Only You Jesus - Gospo Media
Connect with us

Audio: Bliss Asikoko – Only You Jesus

Audio

Audio: Bliss Asikoko – Only You Jesus

Kutoka nchini Nigeria leo nimekuletea wimbo mzuri wa kuabudu uitwao Only You Jesus kutoka kwa mwimbaji aliyepakwa mafuta anayefahamika kwa jina la Bliss Asikoko, muziki huu umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Afor kutoka nchini Nigeria.

Bliss ni mwabudu mwenye upendo kwa Roho Mtakatifu. Utumishi wake umekuwa unaacha alama za miujiza kwa watu, nyimbo zake zinaaminika kuwa zinaongozwa na Roho Mtakatifu na kumtukuza Baba na kuimarisha kanisa.

”Only You Jesus” ni wimbo unaoeleza ukuu na upendo wa Bwana wetu Yesu Kristo kwa yale ambayo ameyafanya kwa ajili yetu, yeye ni shujaa wetu tunalitukuza jina lake kwa dunia yote, yeye ni yule ambaye ameketi katika kiti cha enzi pamoja na Mungu Baba, huyu ni mwanakondoo anayestahili sifa na kuinuliwa.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao nina imani kuwa utakubariki na kukuinua kila wakati unapokuwa unasikikiliza, Ameen.

 

Download Audio

Social Media
Instagram: @bliss_asikoko
Twittter: @bliss_asikoko

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top