Audio Music: Benedict Fanuel - Sababu Bado Naishi - Gospo Media
Connect with us

Audio Music: Benedict Fanuel – Sababu Bado Naishi

Audio

Audio Music: Benedict Fanuel – Sababu Bado Naishi

Kutoka jijini Dar es salaam leo kwa utukufu wa Mungu nimekuletea wimbo uitwao Sababu Bado Naishi kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Benedict Fanuel akiwa chini ya menejimenti ya Balozi wa Vijana Tanzania, wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Jesus Power Records chini ya mikono mahiri ya prodyuza YZ Manamba ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili.

Wimbo huu ni washukrani ukitukumbusha upendo wa Mungu usiofananishwa na kitu chochote katika maisha yetu hata uhai wetu leo ni kwasababu ya uwepo wa nguvu yake na upendo wake mkuu katika maisha yetu, hivyo yatupasa kumshukuru Mungu kwa yote kwa maaana bila yeye sisi si chochote katika kutimiza kusudi aliloliweka ndani yetu.

“Kuna Sababu ambayo imenifanya Niimbe huu wimbo, Maisha yetu ni sababu tosha ya kurudisha utukufu na Heshima kwa Mungu maana yeye ndiye ajuaye kesho yetu ipoje kila jambo ambalo tulifanyalo chini ya jua kuna sababu ambayo Mungu amekwisha iandaa hivyo kuna sababu ya kila mmoja wetu kurudisha sifa na utukufu kwa mungu.

SABABUBADONAISHI ni nyimbo ambayo imebeba ujumbe mzito.. ni nyimbo ambayo inafanya mtu apate tumaini la kuishi.. Nilitunga nyimbo ya SABABU BADO NAISHI kwa sababu nimekuwa nikitafakari sana mambo ambayo Mungu anafanya juu ya maisha yetu ni mambo ambayo tunashindwa kumlipa…..Ametupatia uhai na pumzi ya bure ambayo hatutoi kiasi chochote cha fedha, ametupa uwezo wa kuishi.. ni kwasababu tu ya upendo wake” kwahiyo kila mtu anapaswa atambue kuwa anaishi kwasababu, kuna sababu ambayo inafanya mpaka leo tuko hai Hivyo basi ni jukumu la kila mtu kujua hiyo Sababu inayomfanya aishi……..” – alisema Benedict Fanuel..

Naamini mwana wa Mungu utabarikiwa utakapokuwa unausikiliza wimbo huu utakaokufanya umtafakari Mungu kwa kiwango kingine kwa yale ambayo amekutendea. Karibu upakue na ubarikiwe.

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko wasiliana na mwimbaji Benedict Fanuel kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 713 606 038
Facebook: Benedict Fanuel
Instagram: @benanto_tz
Youtube: Benedict Fanuel

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Audio

To Top