Video

Video: Benachi – Tiba Yangu

Kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Nairobi nchini Kenya anayefahamika kwa jina la Benachi kwa mara ya kwanza kwa mwaka 2018 ameachia video yake nzuri iitwayo Tiba Yangu, Video hii imeongozwa na studio za Trued Pictures na muziki ukiwa umetayarishwa na prodyuza Saint P.

Tiba Yangu ni wimbo wa kukiri ushindi ndani ya Yesu Kristo kwa maana hakuna jambo analoshindwa kwake vyote vinawezekana uponyaji wake na mguso wake katika maisha Yetu ni Tiba tosha kwa mioyo iliyovunjika na kukata tamaa… Hii ni Tiba yangu kwa maana wapo waliosema kuwa msaada upo kwa waganga na wengine wakema pesa ndio tiba tosha lakini kwako nimekwama Baba maana nimeona ukiponya, nimeona ukigusa walemavu wanatembea na vipofu pia wanaona kwako sitoki noo wewe ndiye Tiba Yangu dawa ya nafsi yangu na roho yangu…

Nina hakika utabarikiwa kwa kuitazama video hii na baada ya kupakua wimbo huu utapokea mguso wa pekee wa Tiba ya Bwana wetu Yesu Kristo. Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Benachi kupitia
Facebook: Benachi Mwanake
Instagram: @benachi_mwanake
YouTube: Benachi Kenya

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video: PeaceKing David Feat. Neema Gospel choir - Jesus you are my King

Next post

Video | Audio: Sunny Praise – You Are Beautiful