Audio: Ben William - Wa Moyo - Gospo Media
Connect with us

Audio: Ben William – Wa Moyo

Audio

Audio: Ben William – Wa Moyo

Baada ya kufanya vizuri mwaka 2018 kupitia nyimbo kadhaa alizoziachia ikiwa pamoja na ile iitwayo Nakupenda na Emmanuel, Kwa mara nyingine tena katika mwaka 2019 mwimbaji Ben William kutoka jijini Mwanza ametusogezea wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Wa Moyo, Muziki huu ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Apex Music.

“Wamuabuduo Bwana imewapasa kumuabudu katika Roho na Kweli, Neno la Mungu linasema usipomsifu Mungu atainua hata mawe ili yamsifu, kwanini kusubiri mawe yamsifu Mungu wakati wewe upo hai…. Imba wimbo huu kwa kumaanisha na hakika sifa zako zitafika mbele za Mungu na tarajia kubarikiwa kwa namna ya kipekee sana….. tafakari ni mambo mangapi Mungu amekufanyia bila kusahau Mungu anakaa katika sifa.” – alisema Ben

Hii ni moja kati ya nyimbo ambazo utazifurahia katika mwaka 2019, Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza na hakika utabarikiwa kila wakati, Wa Moyo.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Ben William kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 719 813 124
Facebook: Benny William
Instagram: @bennywilliam_Official
Youtube: Ben William

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top