Connect with us

Video | Audio: Ben Jonathan – Siteketei & Salama (Mashup)

Video

Video | Audio: Ben Jonathan – Siteketei & Salama (Mashup)

Kijana mwenye kipaji cha pekee katika uimbaji wa nyimbo za Injili akifahamika kwa jina la Ben Jonathan leo kwa mara ya kwanza amedhihirisha kipaji chake kupitia video ya wimbo wake mpya uitwao Siteketei ukiwa katika mtindo wa Mushup ikimaanisha wimbo mmoja wenye muunganiko wa nyimbo mbili zilizowahi kuimbwa na mwimbaji maarufu kwa sasa katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania na Afrika mashariki Angel Benard. Video hii imeongozwa na director Chris-Era kutoka studio za CAM-BRO na muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Stino na Ramso wakishirikiana na mpigaji mahiri wa Solo Emma Gripa kutoka ndani ya studio za We Focus Entertainment.

Akizungumza na gospomedia.com kuhusu kuachia wimbo huu mwimbaji Ben Jonathan alikuwa na haya ya kusema:

”Nimeachia wimbo huu kwa ajili ya kuwapa moyo wale walioanguka na kukata tamaa, kwamba hakuna haja ya kukata tamaa wala kuteketea. Inatubidi kumwamini Yesu Kristo pekee kwani yeye ndiye atayekaye tuinua na kutusaidia kusonga mbele katika kila tunalofanya kwa utukufu wa Mungu.” – Alisema Ben

Licha ya uzuri wa uimbaji uliotumika katika wimbo huu lakini pia mpangilio mzuri wa vyombo vya muziki utakufanya ufurahie wimbo huu kwa kiwango cha juu kabisa cha kumtafakari Mungu ili upate kujazwa Imani na matumaini ya kuvuka mahali ambapo umekwama.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki na kukuinua kila wakati utakapokuwa unatazama na kusikiliza. Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Ben Jonathan kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 657 994 800
Facebook: Ben Jonathan
Instagram: @benjonathanm
Twittter: @benjonathanm
Youtube: Ben Jonathan

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Video

To Top