Videos

Music Video | Audio: Beatrice Daniel – Msalaba

Kutoka jijini Dar es salaam leo kwa mara nyingine tena nimekuwekea video nzuri iitwayo Msalaba kutoka kwa mwimbaji aliyewahi kufanya vyema mwaka 2016 kupitia wimbo wake uitwao Nataka Nitoke na huyu si mwingine bali ni Beatrice Daniel, video ya wimbo huu imeongozwa na director Alex Soloko na wimbo ukiwa umetayaarihwa ndani ya studio za Tura Records chini ya mikono ya prodyuza PG.

Akizungumza na gospomedia.com mwimbaji Beatrice Daniel amesema ”Msalaba ni wimbo uonazungumzia jinsi Mungu alivyoonesha pendo lake kwetu sisi watoto wake na mpaka akaamua kumtoa mwanaye Yesu Kristo kuyabeba mateso ya msalaba ili sisi wanadamu tuwe huru jambo hili kwangu linadhihirisha uhalisi wa Mungu kupitia Yesu ambaye alikuja duniani katika hali ya kibinadamu lakini akiwa amebeba kusudi la upendo wa Mungu katika kutuokoa sisi ili tusiangamie katika dhambi…. Tazama Mungu ni pendo alimtoa mwana wake aukomboe ulimwengu ili leo tuwe huru..” – alisema Beatrice Daniel.

Hakika ni wimbo mzuri wa sifa kwa moyo mkunjufu nakukaibisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao nina hakika utakubariki sana. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Beatrice Daniel kupitia
Simu/WhatsApp: +255 714919598, +255 769 344 293
Facebook: Beatrice Daniel
Instagram: @beatrice_daniel
YouTube: Beatrice Daniel

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Audio Music: Eliud Martine Feat Rose Francis - Tulia Kwa Yesu

Next post

Audio Music: Massin - Side