Beatrice Daniel Kuachia Nataka Nitoke Albamu ya DVD - Gospo Media
Connect with us

Beatrice Daniel Kuachia Nataka Nitoke Albamu ya DVD

Habari

Beatrice Daniel Kuachia Nataka Nitoke Albamu ya DVD

Na mwandishi wetu,

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Beatrice Daniel ameweka wazi juu ya uzinduzi wa albamu yake mpya iitwayo Nataka Nitoke ikiwa katika mfumo wa video DVD inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 29.04.2018 kuanzia saa sita mchana mpaka saa kumi na mbili jioni katika kanisa la Christan Life Church lililopo Mbagala Kongowe, jijini Dar es salaam.

Akizungumza na gospomedia mwimbaji Beatrice Daniel amesema kuwa uzinduzi wa albamu hiyo utakuwa ni wa kipekee sana kwasababu utakwenda kugusa maisha ya watu ambao wanahitaji kukomblewa na kuinuliwa kupitia jina la Yesu Kristo.

Uzinduzi wa albamu hiyo utahudhuliwa na Mkuu wa wilaya ya Temeke Mh. Felix Lyaniva, Mbunge wa Jimbo la Mbagala Mh. Issa Mangungu, na Mgeni rasmi atakuwa ni mkurugenzi wa Habari ofisi ya waziri mkuu Bi. Irene Bwire.

Beatrice Daniel, mwimbaji wa nyimbo za Injili ambaye tayari ameshafanya vizuri kupitia nyimbo kadhaa ikiwemo Usiniache, Nataka Nitoke na hivi karibuni  ameachia video yake iitwayo Msalaba, amesema anawakaribisha watu wote kufika katika uzinduzi huo ambao utapambwa na kusindikizwa waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Dar es salaam.

Kama Bado hujaitazama video yake ya Msalaba gospomedia.com inakukaribisha kuitazama hapa chini na kupakua wimbo huu ambao ni imani yetu kuwa utakubariki na kukuinua, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Beatrice Daniel kupitia
Simu/WhatsApp: +255 714 919 598, +255 769 344 293
Facebook: Beatrice Daniel
Instagram: @beatrice_daniel
YouTube: Beatrice Daniel

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Habari

To Top