Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Video | Audio: Baraka Nathan – Shujaa

Video

Video | Audio: Baraka Nathan – Shujaa

Kutoka jijini Dar es salaam leo kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018 nimekusogezea video ya wimbo wenye nguvu ya kukupa matumaini uitwao Shujaa kutoka kwa mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa nyimbo za Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Baraka Nathan. Video hii imeongozwa na director Einxer na muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono yake mwenyewe kutoka studio za One Love.

Akizungumza na gospomedia.com mwimbaji Baraka alisema machache kuhusu ujumbe ulio katika wimbo huu:-

“Shujaa ni wimbo uliobeba ujumbe wa kumpa mtu moyo nakumkumbusha kwamba ingawa anapita katika mapito yaliyo magumu sana namsihi usivunjike moyo na kukata tamaa, atambue kuwa hayo ni ya mapito ya muda aendelee kuamini kuwa yeye ni SHUJAA ipo siku yake itakayobadilisha maisha na utukufu wa Mungu utatukuzwa, Kama neno la Mungu linavyosema “Jifunge upanga wako, ewe shujaa! Wewe ni mtukufu na mwenye fahari.” – Zaburi 45:3.

Kama unapitia magumu ya kiuchumi, magumu ya kudharauliwa, umesoma na haupati kazi, umeolewa na hupati mtoto, hayo yote ni mapito tuu, Yesu alishayamaliza yote pale Goligota na kukufanya #S H U J A A.” – Alisema Baraka.

Nina imani kuwa wimbo huu utakuinua na kukupa nguvu mpya ya kusonga mbele kila wakati utakapokuwa unatazama video hii na kusikiliza wimbo huu, Barikiwa mwana wa Mungu amini siku zote kuwa wewe ni SHUJAA, ameen.

[easy_media_download url=”https://gospomedia.com/wp-content/uploads/2018/04/Baraka-Nathan-Shujaa.mp3″ text=”Download Audio” force_dl=”1″]

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Baraka Nathan kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 672 446 674
Facebook: Baraka Nathan
Instagram: @officialbarakatz | @makalaintertiment
Youtube: Makala Entertainment

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Video

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 10 ON GOSPOMEDIA

SUBSCRIBE

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 12,309 other subscribers

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top