Audio: Baraka Mwampamba - Unadumu Milele - Gospo Media
Connect with us

Audio: Baraka Mwampamba – Unadumu Milele

Audio

Audio: Baraka Mwampamba – Unadumu Milele

Kutoka jijini Dar es salaam kwa mara ya kwanza tunamtambulisha kwako mwimbaji mpya katika huduma ya muziki wa Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Baraka Mwampamba maarufu kama Mr. BM ambaye kwasasa ameachia nyimbo zake mbili mpya moja kati ya hizo ni hii hapa inayobebwa kwa jina la Unadumu Milele, Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za MR. BM Records.

“Namshukuru Mungu sana kwa hatua hii, Wimbo wa UNADUMU MILELE ulinijia nikiwa studio Baada ya kutafakari sana juu ya watu wengi wanaokata tamaa katika maisha yao na kupelekea hata ndoto zao kufa kabisa ndio maana nimesukumwa kuandika wimbo huu ambao kwa hakika utakwenda kuwabadilisha wote watakaousikiliza na ni imani yangu kuwa ndoto zao zitafufuka tena.” – alisema Mr. BM

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu ambao ni hakika kuwa utagusa na kukubariki kwa namna ya kipekee, Ameen.

Kwa watumiaji wa tovuti bonyeza hapa chini:

Download Audio

Kwa watumiaji wa App bonyeza hapa chini:
Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Baraka Mwampamba kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 712 348 701
Facebook: Baraka Mwampamba
Instagram: @baraka_mwampamba

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top