Connect with us

Bahati Simwiche Kuweka Wakfu Albamu Yake Mpya Tarehe 8 Oct. 2017 C.A.G Gongo la Mboto.

Matukio

Bahati Simwiche Kuweka Wakfu Albamu Yake Mpya Tarehe 8 Oct. 2017 C.A.G Gongo la Mboto.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Dar es salaam Tanzania Bahati Simwiche Anatarajia kuweka wakfu albamu yake mpya inayobeba jina la ”Jina la Yesu Kwetu ni Dawa” siku ya jumapili ya tarehe 8.10.2017 ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo saba na itapatikana kwenye mfumo wa Audio CD.

Akiongea na timu ya habari ya gospomedia.com mwimbaji Bahati Simwiche amesema kuwa wakfu wa albamu hiyo itawekwa ndani ya Ibada ya kanisa la C.A.G, Majohe Gongo la mboto kwa mchungaji Amosi Peter Lilai na Ibada hiyo itaanza Saa 4 kamili asubuhi.

Kwa upande wa huduma ya uimbaji katika kusindikiza wakfu wa albamu hiyo mwimbaji Bahati Simwiche amesema ”Waimbaji wengi watakuwepo akiwepo Emmanuel Mbasha, Yvonne Fabian, Beatrice Kitauli, Tumaini Msowoya, Frollence Mackenze, Witness Mbise, Ritha Komba, Mathias Hondwa, Moses Simkoko na waimbaji wengine wengi…” Alisema Simwiche, Hivyo amewaomba wadau na watu wote wanapenda muziki wa Injili kufika siku hii muhimu ambayo itakwenda kuwabariki na kuwainua sana.

Kwasasa mwimbaji Bahati Simwiche Bado anatamba na video yake inayobeba jina la albamu yake tarajiwa ”Jina la Yesu Kwetu ni Dawa” kama ba,do hujawahi kuitazama tunakukaribisha kuitazama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana na usiache kufika siku ya kuweka wakfu wa album hii pale Majohe, Gongo la Mboto katika kanisa la C.A.G kwa mchungaji Peter Lilai. Wote mnakaribishwa!!

Download Audio

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Matukio

To Top