Connect with us

Bahati Simwiche Kuja na wimbo mpya ”NYOTA”

Habari

Bahati Simwiche Kuja na wimbo mpya ”NYOTA”

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Dar es salaam Tanzania, Bahati Simwiche ameweka wazi ujio wa nyimbo yake mpya inayobeba jina la Nyota anayotarajia kuachia mapema mwezi huu, ikiwa ni moja ya wimbo unaopataikana kwenye albam yake mpya iitwayo Jina la Yesu Kwetu ni Dawa ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo saba katika mfumo wa Audio CD iliyozinduliwa na kuwekwa Wakfu Tarehe 8.102017 katika kanisa la C.AG Majohe, Dar es salaam.

Akiongea na gospomedia.com mwimbaji Bahati Simwiche alikuwa na haya ya kusema ”#ASANTE Kwa kuipokea yyimbo ya JINA LA YESU KWETU NI DAWA na kufanyika Baraka ndani yako na kama bado hujaitazama Ingia Sasa Youtube uitazame na usisahau kusubcribe…kwa sasa tegemea kupokea nyimbo mpya toka kwa BAHATI SIMWICHE Iitwayo NYOTA…Mamajusi waliona UZITO wa Ile NYOTA wakaifuata…! Walipita wengi ila ni mmoja tu aliyepata kibali naye alikuwa mawindoni akichunga kondoo…mwisho wa siku akawa Mfalme…#NYOTA 1 Samuel 16 : 11 -13”

Kwasasa mwimbaji Bahati Simwiche bado anatamba na video yake inayobeba jina la albamu yake mpya ”Jina la Yesu Kwetu ni Dawa” leo tunakukaribisha tena kama bado hujawahi kuitazama tunakukaribisha kuitazama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana na endele kusubiri ujio wake mpya wa NYOTA inayotarajiw akuachiwa hivi karibuni kupitia tovuti yako pendwa ya gospomedia.com.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi juu kuipata nakala ya albamu yake mpya na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Bahati Simwiche kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 713 509 221 au +255764509221
Facebook: Bahati Simwiche
Instagram: @simwiche12
YouTube: Bahati Simwiche
Email: simwiche12@gmail.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Habari

To Top