Connect with us

Audio Music: Shalom Obosa – My Case is Different

Muziki

Audio Music: Shalom Obosa – My Case is Different

Kutoka kwa mshindi wa mashindano ya Bezaleel Gospel Music msimu wa saba, akifahamika kwa jina la Shalom Obosa kutoka jijini Kano kaskazini magharibi mwa nchi ya nigeria ameachia wimbo wake mpya wenye kubariki sana uitwao ”My Case is Different” muziki huu umetayarishwa na prodyuza aliyekuwa mshindi wa tuzo mbalimbali nchini humo anayefahamika kwa jina la Timi Toba kutoka ndani ya studio za Just Beat Records.

Mashairi ya wimbo huu sio tu yanadhihirisha kukombolewa kwetu kutoka kwenye vifungo vibaya vya ulimwengu kama watoto wa Mungu lakini pia umeeleza juu ushuhuda wa jinsi sisi ni tulivyoumbwa kuishi kwa furaha duniani kwa nuru ya ahadi nyingi za Mungu katika maisha yetu.

Shalom alisema, “huruma za Mungu juu ya maisha yangu zilinitia moyo kuandika wimbo huu. Neno lake katika Zaburi ya 91 na Malaki 4, imenipa ujasiri mkubwa wa kuendelea katikati ya dhoruba. Pamoja na dhoruba, bado nimesimama… Mungu bado ananilinda. Sura hizo za Biblia zilinipa imani hii kwamba mimi siruhusiwi kuanguka wakati wengine wanaanguka kwa sababu mimi ni wa Mungu mwenyewe na imenifanya kuwa na uwezo wa kushindwa kuanguka katika mfano wa kila changamoto. Siwezi kuanza kusema yote ambayo Mungu amefanya kwa ajili yangu lakini nitakuhesabu kwa kusema kwamba huruma ya Mungu ni ya kweli na haijawahi kushindwa. Natumaini wimbo huu wa ushuhuda unawahimiza kushikilia Imani imara kwa Mungu. Kesi yako itakuwa tofauti mahali pote bila kujali changamoto unazopitia. Mungu akubariki unapokuwa unasikiliza wimbo huu”

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao kwa hakika utakwenda kukuinua na kukubariki sana!!

 

Download Audio

Social Media
Facebook: Shalom Obosa
Instagram: @officialshalom
Twittter: @officialshalom

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

To Top