Connect with us

Audio Music: Piniel Steti – Gusa Pindo

Muziki

Audio Music: Piniel Steti – Gusa Pindo

Kutoka jijini Arusha, leo nimekuletea wimbo mpya kutoka kwa mtumishi wa Mungu, mwimbaji na mtayaarishaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Piniel Steti wimbo huu unaitwa ”Gusa Pindo” ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio yake iitwayo Jibu Media.

Gusa Pindo ni moja ya wimbo unaopatikana kwenye album yake ya sita inayobebwa na jina la ”Injili Inalipa” ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo nane ikiwemo ”Twende Kanisani”, ”Nisikilize”, Karibu Roho n.k

Akiongea na gospomedia.com mtumishi Piniel Steti amesema kuwa wimbo wa Gusa Pindo unazungumzia jinsi Yesu anavyoweza kutenda miujiza mikubwa katika maisha yetu pale tutakapoamua kumwamini, kumfuata na kumkabithi maisha yetu.

”Nimetoa album hii ya Injili Inalipa Baada ya kuona kuwa unaweza kufanya kazi zote duniani ambazo zote zinafaida na hasara lakini kufanya kazi ya Mungu(Uinjilishaji) ni faida bora zaidi kwa yule anayeifanya kwa moyo na kumaanisha kupitia jina la Yesu Kristo”. – Piniel Steti.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu. Karibu ubarikiwe!!

Download Audio

Kwa wasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mtumishi Piniel Steti kupitia:

Simu/WhatsApp: +255 755 024 693, +254 702 924 809
Facebook: Piniel Steti
YouTube: Piniel Steti
E-mail: pinielstetti@gmail.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

TRENDING

To Top