Music

Audio Music: Massin – Side

Side ni wimbo mpya kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini zambia anayefahamika kwa jina la Massin. Wimbo huu umetayarishwa kwenye mahadhi ya Dancehall na Afro ukiwa umetayaarishwa chini ya mikono ya prodyuza Ojo.

Kupitia wimbo huu mwimbaji Massin anamzungumzia Mungu jinsi anavyokuwa upande wake siku zote. Marafiki wanaweza kukuacha, mahusiano yanaweza kuacha matokeo ya chuki lakini upendo wa Mungu umekamilika bila kujali kile kinachoweza kuja kwa njia yake kamwe hawezi kutuacha.

Ukamilifu wa wimbo huu umepatikana kwenye kitabu cha Zaburi 56: 9. nakukaribisha kwa moyo mkunjufu usikilize na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utaufurahia.

 

Download Audio

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Music Video | Audio: Beatrice Daniel - Msalaba

Next post

Music Video | Audio: Neema & Paul - Nitetee