Connect with us

Audio Music: Hellen Sogia – Ndoa Ni Takatifu

Muziki

Audio Music: Hellen Sogia – Ndoa Ni Takatifu

Kutoka kwa mtumishi wa Mungu Nabii Hellen Sogia leo kupitia blog yako pendwa ametuletea wimbo wake uitwao ”Ndoa Ni Takatifu” ikiwa ni wimbo unaobeba jina la album yake ya pili anayotarajia kuachia sokoni pale itakapokamilika.

”Ndoa ni Takatifu”  ni wimbo unazongumzia uhalisia wa maisha ya Ndoa katika kipindi cha kizazi hiki ambapo kumekuwa na masumbufu ya wanandoa wengi katika familia zao hali inayopelekea ndoa hizo kuvunjika na hata kuleta migogoro na mifarakano mikubwa baina ya familia moja na nyingine, hivyo kupitia wimbo huu mtumishi Hellen Segio anatakumbusha thamani ya ndoa katika maisha yetu kuwa imebeba kusudi la Mungu na hivyo inampasa kila mwanandoa kuheshimu ndoa yake kwakuwa Ndoa ni Ibada takatifu ambayo haipaswi kutendewa kinyume na mapenzi ya Mungu.

Mbali ya kuwa mwimbaji Hellen Segio pia ni nabii katika taasisi iitwayo Oak Mission Ministry ikiwa na matawi yake jijini Dar es salaam na Arusha na amekuwa akihudumia nchini mbalimbali ndani nje ya Afrika.

Ewe kijana ambaye una matarajio ya kuwa na ndoa, na wale wote ambao wapo kwenye ndoa wimbo huu wa ”Ndoa ni Takatifu” utakupa ujumbe wenye kukufundisha na kukumbusha juu ya uthamani wa Ndoa katika maisha yetu ikiwa ni sehemu muhimu katika ufalme wa Mungu.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana siku ya leo. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mtumishi Hellen Sogia kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 753 351 048, +255 716 711 867
Facebook: Ap Hellen Sogia

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

To Top