Connect with us

Audio Music: Emmanuel Singano – Alpha & Omega

Muziki

Audio Music: Emmanuel Singano – Alpha & Omega

 

Kutoka kwenye label kubwa kabisa ya Apex Music leo kwa utukufu wa Mungu nimekuwekea wimbo uitwao Alpha na Omega kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Emmanuel Singano kutoka jijini Mwanza. wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Apex Music chini ya mikono bora kabisa ya prodyuza Benny William.

Alpha na Omega ni wimbo wa sifa unaomtukuza Bwana wetu Yesu Kristo kuwa ni mwanzo na mwisho wa vitu na mambo yote duniani na mbinguni, kwa upendo wake kwetu aliamua kufa msalabani ili mimi na wewe tupokee neema ya ukombozi kwa damu yake na hiyo ndiyo alama kuu ya udhihirisho wa kuanza kwa maisha yetu mapya ya utakaso na kufuta zile dhambi zetu za kale, hakuna kinacholizidi jina la Yesu maana vyote kwakwe ni mwanzo na mwisho. Kama bado hujaokoka leo nakupa nafasi ya kusikiliza wimbo huu kwa makini na kuchukua hatua ya kumkaribisha Yesu ndani ya moyo ili afute vifungo vyote vya dhambi zako leo.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu na ni hakika utakwenda kubadilisha maisha yako leo. Karibu ubarikiwe!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko wasiliana na mwimbaji Emmanuel Singano kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 755 931 081
Facebook: Emmanuel Singano
Instagram: @emmanuel_singano_official

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top