Connect with us

Audio Music: Dona JR. Feat John Lihawa, Sunday Mkweli, Gazuko, Bishop Abra, SirMbezi, Miriam Jackson – Sihitaji Refa

Muziki

Audio Music: Dona JR. Feat John Lihawa, Sunday Mkweli, Gazuko, Bishop Abra, SirMbezi, Miriam Jackson – Sihitaji Refa

Shalom mwana wa Mungu leo nimekuletea wimbo uitwao Sihitaji Refa kutoka kwa mtumishi wa Mungu anayefanya muziki wa Injili kwa mtindo wa HipHop huyu si mwingine bali ni Dona JR ambaye kwa mara nyingine tena ameachia wimbo huu ikiwa ni Rmx ya wimbo aliowahi kuuachia mapema mwaka 2016, wimbo huu umewashirikisha waimbaji mbalimbali wa gospel hiphop akiwemo John Lihawa, Sunday Mkweli, Gazuko, Bishop Abra, SirMbezi,  na kwenye kitikio mwimbaji miriam Jackson amekuwa baraka katika kuing’arisha kazi hii.

Sihitaji Refa ni wimbo unaotukumbusha juu kumtegemea Yesu Kristo kwa maana hakuna binadamu mwenye uwezo wa kufanya makuu na maajabu ambayo Bwana Yesu aliyafanya kwa upendo wake kwetu, hivyo wewe ambaye kwasasa upo kwenye shida na mapito mbalimbali wimbo ukutie moyo na kukuinua na uamini Mungu ndiye mkuu wa vyote kupitia jina la Yesu Kristo atakuokoa na hayo ambayo yanakurudisha nyuma katika kazi yako, uchumi wako, ndoa yako, Elimu yako, familia yako na yote ambayo yanakuzunguka.

”Mungu ndiye aliyeifanya milima, na kuumba upepo; ndiye amjulishaye Mwanadamu mawazo yake; ndiye ageuzaye mchana kuwa usiku, na kukanyaga vilele vya dunia. Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina lake!”’ – Amosi 4:13

Wimbo huu umeandaliwa ndani ya studio za Enzi Records chini ya mikono ya prodyuza Amzy kutoka jijini Dar es salaam.

 

Download Audio

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu uliobeba ujumbe mzito kwa ajili yako na hakika utakwenda kukuinua na kukubariki. Karibu!!

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko wasiliana na rapa Dona JR kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 746 083 735, +255 713 02 44 55
Facebook: Donanciano Van Joseph
Instagram: @255dona
Twitter: @255dona
Youtube: DONA Jesus Rapper

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top