Advertisements
Connect with us

Audio Music: Bahati Simwiche Feat Beatrice Kitauli – Nyota

Audio

Audio Music: Bahati Simwiche Feat Beatrice Kitauli – Nyota

Kutoka jijini Dar es salaam leo kwa utukufu wa Mungu nimekusogezea wimbo mzuri uitwao Nyota kutoka kwa mwimbaji anayefanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania akifahamika kwa jina la Bahati Simwiche hapa akiwa amemshirikisha mwimbaji mahiri pia anayefahamika kwa jina la Beatrice Kitauli, wimbo huu umefanyika ndani ya studio za One Love Records chini ya mikono hodari ya prodyuza Baraka Nathan.

Akiongea na gospomedia.com mwimbaji Bahati Simwiche amesema kuwa ameachia wimbo huu ikiwa ni mwendelezo wa kutangaza albamu yake mpya inayofahamika kama Jina la Yesu Kwetu ni Dawa ikiwa tayari imeshazinduliwa na kuwekwa Wakfu Tarehe 8.10.2017 katika kanisa la C.AG Majohe, Dar es salaam.

Albamu hii ina mkusuanyiko wa nyimbo saba ikipatikana katika mfumo wa Audio CD.

Nyota ni wimbo wa pekee uliobeba ujumbe wa matumaini kwako mwana wa Mungu ambaye mpaka sasa umeshakata tamaa katika yale ambayo umetarajia kuyakamilisha lakini bado hujapata mwanga wa kufanikiwa kwa mambo yako iwe ni Ajira, uchumi wako, ndoa yako, familia yako, elimu yako na hata biashara yako, wimbo huu unakuhamasisha kuwa bado nafasi yako ya kufanikiwa ipo katika yale unayoyatarajia unachotakiwa kuzingatia ni wewe tu kuendelea kumtumainia Bwana Yesu kwakuwa ahadi zake ni za kweli kwetu, maana hawai wala hachelewi.. amini nyota yako lazima ing’ae endelea kumwamini Mungu kupitia jina la Yesu Kristo.

”Mamajusi waliona UZITO wa Ile NYOTA wakaifuata…! Walipita wengi ila ni mmoja tu aliyepata kibali naye alikuwa mawindoni akichunga kondoo…mwisho wa siku akawa Mfalme…#NYOTA 1 Samuel 16 : 11 -13” – Bahati Simwiche

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu wenye mafuta ya kukutia moyo na kukubariki na hakika imani yako itakuwa ni yenye nguvu kwa Mungu. Karibu!!

 

[easy_media_download url=”http://gospomedia.com/wp-content/uploads/2017/11/Bahati-Simwiche-Feat-Beatrice-Kitauli-Nyota.mp3″ text=”Download Audio” force_dl=”1″]

Kwa mawasiliano zaidi na mwimbaji Bahati Simwiche, jinsi ya kuipata nakala ya albamu yake mpya na mialiko ya wasiliana naye kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 713 509 221 au +255 764 509 221
Facebook: Bahati Simwiche
Instagram: @simwiche12
YouTube: Bahati Simwiche
Email: simwiche12@gmail.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements

More in Audio

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP TRENDING

Shad B - Mbalii

Audio

Audio: Shad-B – Mbalii

By April 24, 2019

SUBSCRIBE

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 12,283 other subscribers

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kila siku kutoka ndani na nje ya Afrika.

To Top