Connect with us

Audio: Black Samaritan Feat. Eliud Martine – Barua

Audio

Audio: Black Samaritan Feat. Eliud Martine – Barua

Baada ya kimya cha muda wa takribani mwaka mmoja toka alipoachia wimbo wake uitwao Ahadi mwaka 2017,  Mwimbaji wa nyimbo za Injili kwa mtindo wa HipHop maarufu kama Black Samaritan amevunja ukimya kwa kuachia wimbo wake mpya uitwao Barua akiwa amemshirikisha mwimbaji Eliud Martine.

Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Enzi Records chini ya mikono ya prodyuza Amyz.

“Baada ya kutumika kwa kujua au hata bila kujua kwa kazi za shetani inakuja Neema ya kumjua Yesu, anasema mzigo wake ni mwepesi na NIRA yake ni Laini..ndipo yanakuja maamuzi ya kuacha kazi kwa shetani ambazo ujira wake ni mateso ya milele,

Hii ni Barua ya wazi niliyomwandikia shetani kwamba nimeijua kweli ya kristo na nimeamu kuacha kazi yake, Yesu ameniokoa na ameniajiri nifanye kazi yake na ujira ni uzima wa Milele, Neema na Baraka zake.” – alisema Samaritan

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu ambao kwa hakika utaweka jambo jipya na lenye kukubadilisha ndani yako, Amen.

Kwa watumiaji wa tovuti bonyeza hapa chini:

Download Audio

Kwa watumiaji wa App bonyeza hapa chini:
Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na Black Samaritan kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 716 080 838
Instagram: @black_samaritan

Continue Reading
You may also like...
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top