Connect with us

Audio | B Zablon – Vumilia

Muziki

Audio | B Zablon – Vumilia

Kutoka jijini Arusha leo kupitia tovuti yako pendwa ya gospomedia.com nimekuletea wimbo mzuri wenye kutia moyo na tumaini ndani ya moyo wako uitwao Vumilia kutoka kwa muimbaj B Zablon.

Kila siku binadamu tunakutana na changamoto na matatizo mengi ambayo yanatusababisha kushuka moyo na kukata tamaa kabisa lakini leo kupitia wimbo huu wa Vumilia muimbaji B Zablon anakukumbusha kuwa sehemu ya ugumu unayoipitia kwasasa ni ya muda tu, haijalishi umesubiri kwa kiasi gani ila tambua kuwa Mungu ana kusudi la kupita kwako kwenya hali ngumu uliyonayo sasa.

Inawezekana ni uchumi wako upo duni, elimu yako ni kikwazo cha kutopata ajira, ndoa yako imekuwa na majaribu mengi, watoto wako wanakusumbua na vingine vyote vinavyokusumbua fahamu kuwa jibu lipo kwa Yesu peke yake endelea kumuomba ili aweze kutengeneza maisha yako mapya kutoka kwenye huzuni kwenda kwenye furaha na amani isiyo na kikomo..

”Katika wimbo wa Vumilia nimezungumzia mambo ya maisha ambayo tunakutana nayo kama watu wa Mungu kila siku na mengi yakiwa yanahusu maisha yangu halisi pia, ila mwisho wa siku bado naamini nitavuka, nasubiria wakati wangu wa kuinuliwa.” – Alisema B Zablon

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki na kukupa nguvu ya matumaini ya kuendelea kusubiri wakati wako wa ushindi huku ukimwomba Yesu akupe nguvu ya kushinda vita unayopigana. Barikiwa!

Kwa mawasiliano zaidi:
Simu/WhatsApp: +255 764 257 328 au +255 719 842 139
Facebook: B Zablon Senior
Instagram: @b_zablon_senior
YouTube: B Zablon senior

Advertisement

TRENDING

To Top