Connect with us

Audio: Ajuwae Onesmo – Wengi Wamejisahau

Muziki

Audio: Ajuwae Onesmo – Wengi Wamejisahau

Bwana Yesu asifiwe!! leo kwa utukufu wa Mungu nimekuwekea wimbo wenye ujumbe wa kipekee uitwao Wengi Wamejisahau kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili kutoka jijini Mwanza anayefahamika kwa jina la Ajuwae Onesmo, wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Exodus chini ya mikono ya prodyuza Gilbert Noah ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili.

Katika maisha yetu tumepata kushuhudia watu mbalimbali waliopata kubarikiwa kwa kuinuliwa katika maisha yao lakini wamekuwa wanatenda kinyume na mapenzi au kusudi la Mungu juu ya kuinuliwa kwao na kupelekea kuwatendea wengine vibaya kwa kuwatenga, kuwasengenya na kutowapa msaada kwa wenye uhitaji, jambo hili limekuwa linaathiri sana familia zetu na hata jamii kwa ujumla lakini leo mtumishi Ajuwae Onesmo anatukumbusha kuwa pale ambapo tunainuliwa basi ni vyema tukatambua kuwa ni kwa makusudi ya Mungu kwamba umefanyika baraka na daraja la watu wengine ambao unatakiwa kuwasaidia ili nao wadhihirishe wema wa Mungu maishani mwao.

Hakika hii ni moja kati ya nyimbo nzuri sana iliyobeba ujumbe wa kufundisha na kutukumbusha juu ya upendo kwa wengine hasa pale tunapoinuliwa na kuwa katika nafasi nzuri ya kuwasaidia wengine.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakufunza na kupanda jambo jema katika maisha yako. Karibu ubarikiwe!!.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Ajuwae Onesmo kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 758 576 605
Facebook: Ajuwae Onesmo

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top