Advertisements
Connect with us

Video | Audio: Atosha Kissava – Usisahau Ulikotoka

Audio

Video | Audio: Atosha Kissava – Usisahau Ulikotoka

Baada ya kufanya vizuri sana kupitia video ya wimbo uitwao Nakuamini Mungu aliyoiachia mwezi Machi 2018 mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Atosha Kissava kwa mara nyingine tena ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao Usisahau Ulikotoka.

Video hii imeongozwa na director  Traveller kutoka Kwetu Studios na Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa chini ya mikono ya prodyuza PG.

Usisahau Ulikotoka ni wimbo uliojaa mafundisho yenye kutukumbusha na kutusihi juu ya kuwa na unyenyekevu kwa watu ambao wametusaidia kupata mafanikio au kupiga hatua moja kwenda nyingine katika mafanikio hayo.

Ipo faida ya kunyenyekea na kutosahau tulipotoka ili nguvu ya Baraka na muujiza wetu uwe wa kudumu, Kila wakati wakumbuke waliokusaidia haijalishi una nafasi gani kubwa mpaka hapo ulipofika, Kwa maana Mungu hutumia watu kuinua watu ipo faida kumshukuru Mungu na kurudisha fadhila kwa wote waliokunyanyua na kukusaidia kufika hapo ulipo.

Ni imani yetu kuwa wimbo huu utakuwa ni wenye kugusa, kubadilisha na kuimarisha upendo na unyenyekevu ndani yako, Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii na hakika utabarikiwa!

[easy_media_download url=”https://gospomedia.com/wp-content/uploads/2018/09/Atosha-Kissava-Usisahau-Ulikotoka.mp3″ text=”Download Audio” force_dl=”1″]

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Atosha Kissava kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 719 926 175
Facebook: Atosha Kissava
Instagram: @atoshakissava
Youtube: Atosha Kissava Official

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP TRENDING

Shad B - Mbalii

Audio

Audio: Shad-B – Mbalii

By April 24, 2019

SUBSCRIBE

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 12,283 other subscribers

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kila siku kutoka ndani na nje ya Afrika.

To Top