Audio

Audio: Asha Elia – Walk Together

Kutoka jijini London Uingereza leo tumekusogezea wimbo mpya uitwao “Walk Together” Kutoka kwa mwimbaji anayefahamika kwa jina la Asha Elia, Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa chini ya mikono ya prodyuza IVN.

“Niliandika wimbo baada ya kupita katika jaribu ambalo naamini kabisa kwamba ni Mungu pekee aliyenitetea, Natambua kuwa mtu atabaki kuwa mtu tu, Kuna muda ilinibidi kuachilia uhusiano wangu uvunjuke kwa kuwa naamini Mungu aliniongoza kuchukua muda na kutafuta uthibitisho zaidi kutoka kwake.

“Ilikuwa ngumu, lakini nilijua kuwa kitu chochote nje ya mapenzi ya Mungu hakiwezi kufanya kazi .. Huu ni mtazamo wangu juu ya Ufalme na moyo unaompa Mungu upendo na heshima, Kwakuwa ni Yeye tu anayestahili.” – Asha Elia

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu ambao ni imani yetu kuwa utakubariki, Amen.

Download Audio

Social Media
Facebook: Asha Elia
Instagram: @ashaelia
Youtube: Asha Elia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Mc Freddie - Amen

Next post

Audio: Amanda Ofori - Majesty