Article: KUNA TOFAUTI KUBWA KATI YA MTU NA KOSA..By Sam Sasali - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Article: KUNA TOFAUTI KUBWA KATI YA MTU NA KOSA..By Sam Sasali

Maarifa

Article: KUNA TOFAUTI KUBWA KATI YA MTU NA KOSA..By Sam Sasali

Kosa ama Makosa Ya Mtu Sio Mara Zote Yanamueleza Mtu Huyo Alivyo.
Umewahi sikia mtu anasema “Nilikuamini sana sikujua kama uko hivi tusijuane kabisa”. Kuna watu ambao kimsingi “Sivyo Walivyo” ila kuna mambo pengine ndiyo yamepelekea pengine wafanye wanayoyafanya ambayo kimsingi sio wao ila pengine Msongo wa Mawazo.
Nimekaa na Milembe Mke wangu miaka michache nimejifunza kuna mambo ambayo kimsingi ndiyo yanayomfanya awe yeye na nina kazi ya kumfanya yeye kuwa yeye na iwapo ikatokea kuna kitu nikagundua tiba sio Lawama ila Msaada wa kuendelea kumfanya yeye kuwa yeye. Nami kadhalika.
Kuna watu ambao tumewafahamu ama tumefahamiana kitambo mfano. Mimi na Swahiba wangu Prosper Mwakitalima kuna vitu akifanya basi sina budi kujua “huyu ni Prosper” “huyu Sio Prosper” ikitokea leo nikisikia Prospet anapigana na mtu ama wanabishana kwa matusi. Siwezi sema “kumbe ndo ulivyo….loooh”.
Mara nyingi sanaa watu wakifanya makosa ni mara chache sana kuna watu wanaweza tofautisha “Kosa”….na “Mtu”. Kumlaumu ama kumshutumu mtu kwa kosa alilolifanya wakati mwingine ni Kumtonesha jeraha la moyo wake. Ikitokea dada yako amepata ujauzito nje ya ndoa pengine badala ya kumlaumu ni vema ukamsaidia. Kumlaumu hakutamfanya kurudi hali yake ya kabla ya Kosa. Wakati mwingine ni vema ukatafuta muda kufahamu nini kilipelekea kufikia katika Kosa na kumsaidia asidondokee katika kosa tena.
Badala ya Kulaumu tujifunze kusaidia pale unapoona mwenzi wako,Kiongozi wako,rafiki yako ama mtu yeyote anatoka nje ya Mstari.
‪#‎ThoughtsActivated‬#
Source: Samuel Nathaniel Sasali facebook page

Continue Reading
You may also like...

More in Maarifa

To Top