Audio: April Mo – Remember - Gospo Media
Connect with us

Audio: April Mo – Remember

Audio

Audio: April Mo – Remember

Kutoka nchini Nigeria leo nimekusogezea wimbo mzuri uitwao Remember kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la April Mo, Muziki huu umetayaarishwa na prodyuza Eli J na kurekodiwa ndani ya studio za TPG zilizopo nchini Nigeria.

“Kumbuka mambo niliyoyafanya zamani. Mimi ni Mungu wa pekee, na hakuna kama mimi, Ninayeweza kukuambia yatakayojiri kwa siku zako zijazo kabla hata hazijatokea. Kila kitu ninachopanga lazima kitatokea, kwa maana mimi hufanya chochote ninachotaka “.

Wakati mwingine unaweza kuhuhisi kama hakuna kitu kinachofanyika! Vikwazo vya maisha hujaribu kukupima na kukushusha chini, Lakini nakusihi usiondoe imani, Kumbuka Yeye ni Yesu wa Jana, Leo na hata Milele.

Bwana ni mwaminifu katika kutimiza ahadi zake, kama wengine wanavyohesabu miaka, kwake ahadi zake hutimiza ndani ya siku moja tu, Yesu anakujali, usikate tamaa simama imara, kwakuwa Bwana ana mpango mwema na wewe.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza wimbo huu na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana.

 

Download Audio

Social Media
Instagram: @_aprilmo
Twittter: @_aprilmo

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top