Video

Music Video | Audio: Angel Magoti – Fuata Njia

Baada ya kimya cha muda mrefu mwimbaji mwenye kipawa cha hali ya juu cha sauti Angel Magoti leo kwa mara ya kwanza kupitia tovuti yako pendwa ya gospomedia.com nimekusogezea video yake nzuri iitwayo Fuata Njia ikiwa imeongozwa na director Jackson Joackim kutoka studio za Blessing na muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya stuzio za Vocapela chini ya mikono ya prodyuza Steve White.

Fuata Njia ni wimbo uliobeba ujumbe wa kutukumbusha juu ya kumkiri na kufuata njia na  matendo ya Bwana wetu Yesu Kristo katika maisha yetu kwa maana uzima wetu, mafanikio yetu na chochote tunachohitaji kipo ndani ya uwezo wake na nguvu zake, kama bado unajitafakari juu ya kurudi kwa Yesu basi fanya uamuzi huo leo kwa kufuata njia ya Yesu kikamilifu na hakika utaokolewa na kuinuliwa.

”Bwana ndiye mchungaji wangu. Taa na Ngome yangu. Ni kwake Yesu peke yake ndiko kwenye Amani ya kweli. Ukiifuata njia yake utabarikiwa,utaokolewa,utapata uponyaji,utapata Amani ya kweli lakini kikubwa zaidi Utapata Uzima Wa Milele. FUATA NJIA YA BWANA YESU.” – Angel Magoti

Huu ni wimbo wa pekee ambao utakujaza baraka na nguvu ya kumtafakari Mungu kwa upya na kufanya maamuzi ya kumkabithi Yesu maisha yako leo. Karibu utazame video hii na kupakua wimbo huu ambao utakwenda kuweka neno jipya katika maisha yako leo. karibu!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko ya huduma wasiliana na muimbaji Angel Magoti kupitia
Simu/WhatsApp: +255 714 531 444
Facebook: Angel Danny Magoti
Instagram: @angelmagoti
YouTube: Angel Magoti
Twitter: Angel Magoti

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Music Audio: Joyce Omondi - Perfect Gift

Next post

Music Audio: Paul Shole - Safari