Connect with us

Mwimbaji Angel Bernad Apata Mtoto wa Kike

Habari

Mwimbaji Angel Bernad Apata Mtoto wa Kike

Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania anayefanya vyema katika kiwanda cha muziki wa Injili afrika mashariki Angel Bernad leo amebarikiwa kujifungua mtoto wa kike katika hospitali ya MountMeru mkoani Arusha, habari hii njema imethibitishwa na mume wa mwimbaji huyo Bw.Godsave Sakafu kupitia ukurasa wake wa facebook saa chache zilizopita akisema:

Hii ni baraka na furaha kubwa kwa wanandoa hawa ambao wamepata kibali kikubwa katika tasnia ya uimbaji wa muziki wa Injili nchini Tanzania wakiwa wanafanya vyema sana kupitia kazi zao na huduma zao wanazoendelea kuzifanya ndani na nje ya Tanzania zikiwa zinaachilia baraka nyingi kwa watu wanaowafuatilia.

Katika pozi, Bw.Godsave Sakafu akiwa na mke wake Angel Benard

Ikumbukwe kuwa huu ni uzao wa pili kwa mwimbaji Angel Bernad akiwa na mume wake Godsave Sakafu huku mtoto wao wa kwanza akiwa ni wa kiume anayefahamika kwa jina la Bracha Testimony(BT).

Bracha Testimony(BT)

Uongozi na timu nzima ya wanahabari wa gospomedia.com tunatoa pongezi kwa familia ya Bw.Godsave Sakafu na Bi.Angel Benard kwa kupata mtoto mwingine ambaye tunaamini atakwenda kuwa baraka katika familia hii Mungu azidi kuwatumia na kuwainua.

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Habari

To Top