Audio: Angel Benard - Utukumbuke - Gospo Media
Connect with us

Audio: Angel Benard – Utukumbuke

Audio

Audio: Angel Benard – Utukumbuke

Mara baada ya kufanya vizuri kupitia wimbo wake uitwao Jana Leo aliouachia miezi michache iliyopita mwimbaji mahiri na anayefanya vizuri sana katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania na Afrika Mashariki Angel Benard amekuja tena na wimbo wake mpya na wenye kuinua uitwao Utukumbuke ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Still Alive zilizopo jijini Nairobi nchini Kenya.

Utukumbuke ni wimbo unaoelezea maombi kwa Mungu juu ya yale tunayoyahitaji katika maisha yetu, Wanadamu leo tumekuwa tunapita katika majaribu magumu na shida mbalimbali ambazo kwa wakati mwingine zinatufanya tuwe mbali na uso wa Mungu lakini mwimbaji Angel Benard kupitia wimbo huu anatukumbusha kuwa licha ya kila majaribu na shida zote tunazopitia bado Mungu ana nafasi ya kutusikiliza kwa kile tunachohitaji kutoka kwake kwa maana mkono wake sio mfupi usiokoe na sikio lake sio zito asisikie yeye ni mwanzo na mwisho kwake hakuna linalomshinda Bwana Yesu.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki na kukuinua siku zote, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi, mialiko ya huduma wasiliana na muimbaji Angel Bernad kupitia
Simu/WhatsApp: +255 652 887 050 au +255 759 444 488
Facebook: Angel Benard
Twitter: @angelbenard
Instagram: @angelbenardofficial
YouTube: Angel Benard

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Audio

To Top