Connect with us

Music Audio: Angel Benard – Jana Leo

Muziki

Music Audio: Angel Benard – Jana Leo

Mara baada ya kufanya vizuri sana kupitia video yake iitwayo Siteketei ambayo mpaka sasa inaendelea kufanya vyema na kuzidi kubariki watu wengi zaidi. Leo kwa mara nyingine tena muimbaji mahiri na mwenye mafuta ya pekee katika kumtumikia Mungu kwa njia ya muziki wa Injili Angel Benard ametuletea tena wimbo wake mzuri na wenye kubariki mno uitwao Jana Leo.

Jana Leo ni wimbo wa shukurani unaozungumzia nguvu ya maisha ya mtu kwa yale aliyopitia kwa siku za nyuma na leo ambapo maisha ya mtu huyo yanaonekana kubadilika inawezekana kuna vitu ambavyo kwa siku za nyuma vilikusumbua na kukutesa lakini kumbuka ulikuwa unawaza kesho yako itakuaje na leo tayari imeshafika lakini mambo bado hayajabadilika au yameshabadilika kwa hali yoyote uliyonayo leo kumbuka kumshukuru Mungu kwa yote kwakuwa yeye pekee ndiye mwenye nguvu ya kuendelea kukufanya kuwepo hapo ulipo au kukupelekea mahali pengine ambapo yeye atataka uwepo.

Hakika hii ni moja kati ya nyimbo ambazo zitakupa nguvu ya matumaini na kumtafakari Mungu katika yale ambayo umepitia jana na utambue kuwa leo ni siku nyingine mpya ambayo inaweza kukupa ushindi pale tu utakapoamua kumtegemea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako, Mshukuru Mungu kwa siku ya jana kwa maana yawezekana ilikupitisha katika majaribu na changamoto nyingi lakini kama mpaka leo una pumzi ya uhai amini Mungu ana mpango na wewe furahi na uamini kuwa leo ndipo ushindi wako utapatikana kwa Jina la Yesu.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki na kukuinua mno. Karibu!!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi, mialiko ya huduma wasiliana na muimbaji Angel Bernad kupitia
Simu/WhatsApp: +255 652 887 050 au +255 759 444 488
Facebook: Angel Bernad
Twitter: @angelbenard
Instagram: @angelbenardofficial
YouTube: Angel Bernad

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top