Angel Benard Atwaa Tuzo, Sauti Awards 2018 - Gospo Media
Connect with us

Angel Benard Atwaa Tuzo, Sauti Awards 2018

Habari

Angel Benard Atwaa Tuzo, Sauti Awards 2018

Na Mwandishi wetu.

Habari njema kwa Angel Benard akiwa moja kati ya waimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchini Tanzania na Afrika Mashariki, Kwa mara ya kwanza ameweka historia katika huduma ya muziki wa Injili Tanzania kwa kufanikiwa kutwaa tuzo ya Mwimbaji Bora wa kike Afrika mashariki, Magharibi na Kati (Female Artist of the Year East/West/Central) kwa mwaka 2018 katika za tuzo za muziki injili zinazofanyika nchini marekani kila mwaka maarufu kama Sauti Awards.

Katika kipengele hicho mwimbaji Angel Benard alitajwa na kuwa kwenye orodha na waimbaji wengine mahiri kama vile Celestine Donkor kutoka nchini Ghana, Alice Kimanzi kutoka nchini Kenya, Evelyn Wanjiru kutoka nchini Kenya, Deborah Lukalu kutoka nchi ya Kidemokrasia ya Kongo na Ada kutoka nchini Nigeria.

Hii ni tuzo ya kwanza ya kimataifa kwa mwimbaji Angel Benard, Ikiwa ni mara ya pili kwa nchi ya Tanzania kung’aa katika tuzo hizo ambapo mwaka 2017 tulishuhudia mwimbaji Goodluck Gozbert akitwaa tuzo hiyo kama mwimbaji bora wa kiume kwa mwaka 2017.

Waimbaji wengine ambao wamefanikiwa kutwaa tuzo hizo ni pamoja na Mireille Baswira kutoka nchini Kenya akiwakilisha ugenini amepata tuzo ya wimbo bora wa mwaka, Evelyn Wanjiru kutoka nchini Kenya ambaye amepata tuzo ya wimbo bora wa kuabudu(Worship Song of the Year), Pompi kutoka Zambia ambaye amepata tuzo ya Video bora ya mwaka (Video of the Year West/East Africa), Zangi Alex kutoka Kenya amepata Tuzo ya mwimbaji bora wa kiume ugenini (Male Artist of the Year – Diaspora), Levixone kutoka nchini Uganda akiwa ni Mwimbaji bora wa kiume Afrika Mashariki, Jimmy D Psalmist kutoka nchini Nigeria amepata tuzo ya Wimbo bora wa Hamasa(Inspiration song of the Year), Proud Refuge rapa kutoka Kenya anayeishi nchini marekani amepata tuzo ya wimbo bora wa HipHop, Dj Kamfy amepata tuzo ya Dj bora ugenini(Dj of the Year-Diaspora), Dj Mo kutoka nchini kenya amepata tuzo bora ya Dj Afrika mashariki(Dj of the Year – East Africa), Semiyan & Emmy Kosgei kutoka nchini Kenya wamepata tuzo ya Collabo bora ya mwaka, Tuzo ya Kundi bora la Mwaka imeenda kwa Neema Youth, Collabo bora ya mwaka afrika mashariki imeenda kwa Moji ShortBabaa.

Sauti Awards ni tuzo zinazoandaliwa na kutolewa kila mwaka nchini marekani chini ya taasisi ya Sauti One kwa waimbaji wa muziki wa Injili waliofanya vizuri zaidi Afrika, Na huu ni msimu wa tatu kwa tuzo hizi ambazo zimefanyika tarehe 28 Julai 2018 katika ukumbi wa kanisa la Riverstone Church nchini Marekani.

Uongozi na timu nzima ya Gospo Media inayofuraha kuchukua nafasi hii kutoa pongezi kwa Mwimbaji Angel Benard kwa kuiwakilisha vyema Tanzania katika huduma ya muziki wa Injili, Mungu aendelee kumbariki mtumishi wake.

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Habari

To Top