Angel Benard atajwa katika tuzo za AGMMA, Uingereza - Gospo Media
Connect with us

Angel Benard atajwa katika tuzo za AGMMA, Uingereza

Habari

Angel Benard atajwa katika tuzo za AGMMA, Uingereza

Na Mwandishi wetu,

Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili Angel Benard amekuwa mmoja wa waimbaji kutoka Tanzania waliotajwa kuingia katika kinyang’anyiro cha tuzo kubwa zaidi Afrika zinazofahamika kwa jina la “The African Gospel Music and Media Awards (AGMMA)” nchini uingereza ambazo zinatarajiwa kufanyika tarehe 02.06.2018 katika ukumbi wa East London Arts & Music (ELAM) mjini London, uingereza.

Mwimbaji Angel Benard amechaguliwa katika kipengele cha saba cha tuzo hizo kiitwacho “Artiste of Excellence East Africa(Msanii bora afrika mashariki)” akifuatiwa na waimbaji wengine kutoka Kenya, Uganda na Ethiopia akiwemo Mercy Masika (Kenya), Emmy Kosgei (Kenya), Size 8 (Kenya), Emmy Kosgei (Kenya), Levixone – (Uganda), Baby Gloria – (Uganda), Coopy Bly – (Uganda), na Dawit Getachew ( Ethiopia).

Mbali na mwimbaji Angel Benard waimbaji wengine kutoka Tanzania ambao wamechaguliwa kuingia katika kipengele hicho ni Christina Shusho pamoja na Rose Muhando.

The African Gospel Music and Media Awards (AGMMA) ni tuzo za kipekee za injili zinazotambua talanta kubwa ya injili iliyopo ndani ya muziki wa injili Afrika na vyombo vya habari vya kikristo, na kuvipa heshima.

Lengo kuu la Tuzo hizi ni kuinua na kuhamasisha wanamuziki wa nyimbo za Injili na vyombo vya habari ili kuongeza ubora katika huduma zao, biashara, na kuwa watoaji wa huduma bora katika ufalme wa Mungu.

Tuzo za AGMMA zimeandaliwa na kutayaarishwa na kampuni ya 1615 Media, yenye makao makuu yake nchini uingereza ikijihusisha na uandaaji wa matamasha, na uhusiano wa kimataifa katika sekta ya vyombo vya habari na muziki wa Injili.

Kupitia ujumbe wake mfupi Angel Benard aliandika:-

“Shalom ndugu yangu!
Nimetajwa kuwa katika Tuzo za African Gospel Music and Media Awards za nchini UK, nikitajwa kuwa muimbaji kutoka Afrika Mashariki anayefanya muziki wa Injili kwa namna ya Ubora.

Ombi langu kwako ni kama unakubaliana na jopo hili la majaji, tafadhali ingia katika link hii hapa na kubonyeza mahali penye jina langu. Hapo utakuwa umenitambua kuwa nafaa kuwa katika nafasi hiyo, Asante na Mungu akubariki.” – alisema Angel Benard

Sasa unaweza kumpigia kura mwimbaji Angel Benard ili aweze kuipata Tuzo hii na kuiwakilisha Tanzania kwa kubonyeza hapa chini na Mungu akubariki.

PIGA KURA HAPA

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Habari

To Top