Video

Video | Audio: Andrew Robinson – Ni Neema Yako

Baada ya kufanya vizuri kupitia wimbo wake mzuri wa kuabudu uitwao Nipo Tayari mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili anayefahamika kwa jina la Andrew Robinson ameachia video yake mpya iitwayo Ni Neema Yako. Video ikiwa imeongozwa na director John Maulid kutoka studio za JM production na muziki ukiwa umetayarishwa na mikono ya prodyuza Alex lobulu kutoka studio za AFLOB zilizopo jijini Arusha.

”Ni Neema ya Mungu tu kwa hivi tulivyo leo kulingana na status(nafasi) zetu kila mmoja ni kwa kusudi la MUNGU ndilo linalotufanya tunaishi leo…. ametutoa mbali tumeacha wengi, tumevuka mengi pia, ametuokoa na hasira za adui zetu zaburi 138:7-8, zaburii 139:5…….BWANA ananivumilia kila siku, kila saa yeye ni mwaminifu kwetu kila wakati Mungu anafanya yote haya kwetu sio kwamba sisi ni wema sana bali ni kwa neema na rehema zake tuu….. Yote haya ni kwa wema wake MUNGU kwetu sifa na heshima zote tunarudisha kwake.” – Alisema Andrew Robinson.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii njema na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki kila siku, kila wakati utakapokuwa unausikiliza.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Andrew Robinson kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 765 377 611
Facebook: Andrew Robinson
Instagram: @andrewrobinson
Email: andrewrobinson@gmail.com

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Paul Payne837 Feat. DJ Victor256 - Nakana

Next post

Audio: Julian Roberts - Read All About it(Cover)