Audio: Ambwene Mwasongwe-Tumekubalika - Gospo Media
Connect with us

Audio: Ambwene Mwasongwe-Tumekubalika

Audio

Audio: Ambwene Mwasongwe-Tumekubalika

Baada ya kufanya vizuri kupitia wimbo wake uitwao Jiwe aliouachia mwezi Mei, Mwimbaji mkongwe katika kiwanda cha muziki wa nyimbo za Injili Tanzania maarufu kama Ambwene Mwasongwe kwa mara nyingine ameachia wimbo wake mpya uitwao Tumekubalika.

CHANZO CHA WIMBO TUMEKUBALIKA Miaka mitatu iliyopita nilibahatika kusoma hotuba ya Waziri mkuu wa Israel Netanyahu, na sehemu kubwa ya hotuba yake ilikuwa inajibu maadui zao ambao wamewahi kutamka maneno ya vitisho juu yao, nadhani tunafahamu moja ya maneno maarufu ni ” tutaifuta Israel kwenye ramani ya dunia” Katika kujibu hayo alinukuu andiko toka zaburi 121:4 Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli. 5 BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume. Akawakumbusha adui zao kuwa sisi Israel tulipona kwa Farao ugenini, na tulisurvive Babel kama taifa, tuliishi jangwani tukiwa hatuna shamba wala mbegu lakini tulikula, tumewahi kushinda vita tukiwa bila silaha, (kwa nyimbo) na akaongea maneno mengi mazuri, ya ujasiri na KUKIRI KAMA KIONGOZI KUWA WAMESURVIVE HADI LEO KWA SABABU YA MLINZI WAO ASIYESINZIA( JEHOVA) (kumbuka 2018 Israel inatimiza miaka 70 tangu warudi tena katika nchi yao, wanaofuatilia wanaelewa lugha hii ya kinabii) Maneno haya yalinisaidia sana na kunitia nguvu sana, nikajiona ninaweza kukabili magumu yangu pia maana Mlinzi wangu hasinzii, Mungu akanipa wimbo. VERSE YA KWANZA ( Hesabu 24:8) Mungu amemleta kutoka Misri, Ana nguvu mfano wa nguvu za nyati; Atawameza mataifa walio adui zake, Ataivunja mifupa yao vipande vipande. Atawachoma kwa mishale yake. VERSE YA PILI ( SEHEMU KUBWA MANENO YA NETANYAHU mengine ubunifu wa utunzi tu) Tulipona kwa Farao tukiwa ugenini…. Hatukufa kwa njaa, tukiwa hatuna kitu… Tulinusurika vita, tukiwa hatuna silaha… VERSE YA TATU Ni ufunuo wa kimaandiko, Tulikula mtama kwa maji, tukanawiri kuliko wao ( Shadraka, Meshaki na Abednego)…. Hatukupambwa kama wao, tukapendeza zaidi yao ( Esta) Walitubadilisha majina, Hawakubadili hatima( Eliya Mtaabishaji, Shadraka, Meshaki, na Abednego na wengine wengi) Walipotutupa shimoni, tukaibukia ikulu ( Yusufu) Kule walikotusukumia, ndiko Mungu hupumzikia( kisa cha wakoma wanne, Eliya na Kunguru) Walidhani wanatukimbiza, kumbe wanatusindikiza ( Israel akivuka bahari ya Shamu kukimbia jeshi la Misri)

A post shared by ambwene mwasongwe (@ambwenemwasongwe_official) on

Hii ni moja kati ya kazi ambazo zina ujumbe mzito na wa pekee kutoka kwa mtumishi wa Mungu ambwene tukiamini kuwa itakubariki na kukugusa kwa namna ya pekee sana.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kupakua wimbo huu na hakika utabarikiwa kila wakati utakapokuwa unasikiliza, Barikiwa.

Download Audio Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Ambwene Mwasongwe kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 767 619 931
Facebook: Ambwene Mwasongwe
Instagram: @ambwenemwasongwe_official
Youtube: Ambwene Mwasongwe

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top