Habari

AMBWENE MWASONGWE AWAJIA JUU WANAOWAKATAZA WAIMBAJI WA GOSPO KUIMBA MAANDIKO

Katika hali isiyo ya kawaida mwimbaji wa gospo Tanzania Ambwene Mwasongwe ametoa onyo kwa wadau wachache wa muziki wa injili ambao amewaita wahuni wanaowashawishi waimbaji wa muziki wa injili kutotaja jina la Yesu au maandiko matakatifu kwenye nyimbo zao ili waweze kutoboa kwenye muziki.

Ambwene Ameyaandika hayo kupitia ukuta wake wa FaceBook na kuwataka waimbaji hasa wanaochipukia kuwa makini kwani tupo kwenye kipindi kinachohitaji maandiko kuliko wakati mwingine wowote.

Shalom! Kumekuwa na wahuni wengi siku hizi wanawaharibu watumishi wa Mungu, hasa waimbaji wanaoanza kuchipuka kwa kuwaambia wasiimbe jina la Yesu na wasiimbe maandiko. Eti kwa kisingizio cha kutoka maana watu hawapendi maandiko na hawapendi nyimbo zinazomtaja taja Yesu! Napenda kuwatia moyo waimbaji wote wa injili Tanzania mlioamua kutumika kaeni huu ni wakati sahihi na muhimu sana kuliimba jina la Yesu na kuimba maandiko kuliko wakati mwingine wowote na kila atakayefanya hayo Mungu atamkuza na kumwinua juu sana kuzidi maneno ya hawa wahuni! Pia nawaonya wanaowapotosha waimbaji hawa washindwe kwa Jina la Yesu. Kila atakayepata ujumbe huu amtie moyo mwimbaji wa karibu yake kwa kumwambia Yesu ni jiwe letu la pembeni. Amen” ameandika mwimbaji huyo ambaye ametamba sana na kibao chake cha Upendo.

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
Previous post

VIDEO: JESSICA BM AONGELEA KUFANYA KAZI NA PAUL CLEMENT NA SIFA ALIZOMWAGA KWAKWE.

Next post

MUSIC VIDEO: ANNA BONEKA-TANZANIA