Connect with us

Ambwene Mwasongwe afunga ndoa rasmi

Habari

Ambwene Mwasongwe afunga ndoa rasmi

Muimbaji mahiri na mkongwe katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania Ambwene Mwasongwe jana tarehe 15.04.2018 aliandika historia katika maisha yake baada ya kufunga ndoa rasmi na aliyekuwa mpenzi wake ambaye kwasasa ni mke wake halali wa ndoa.

Kupitia ukurasa wake wa instagram muimbaji Ambwene Mwasongwe aliandika ujumbe wa kumpongeza mpenzi wake huyo kwa safari ndefu waliyotoka mpaka kufikia hatua hiyo kubwa katika maisha yao baada ya kufanyika kwa sherehe ya kumuaga(send-off) siku tatu zilizopita kabla ya kufunga ndoa yao rasmi siku ya jana.

“Nakupongeza mpenzi wangu kwa hatua hii kubwa uliyofikia Jana. Safari ya uchumba miaka minne haikuwa ndogo. Hata sasa Bwana amekusaidia, naamini harusi yako tar 15 April jumapili itakuwa na baraka zaidi. ” – Ambwene Mwasongwe

Hakika jana ilikuwa siku ya baraka sana kwao na kwa niaba ya uongozi wa gospo media tunatoa pongezi zetu za dhati kwa muimbaji Ambwene Mwasonge pamoja na mke wake kwa kufanikisha hatua hii kubwa katika maisha yao, Mungu azidi kumulika taa ya baraka katika maisha yao na familia yao kwa ujumla wake. Ameen.

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Habari

To Top